Job 8:3-7

3 aJe, Mungu hupotosha hukumu?
Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki?
4 bWatoto wako walipomtenda dhambi,
aliwapa adhabu ya dhambi yao.
5 cLakini ukimtafuta Mungu,
nawe ukamsihi Mwenyezi,
6 dikiwa wewe ni safi na mnyofu,
hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako,
na kukurudisha katika mahali pako pa haki.
7 eIjapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo,
lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio.
Copyright information for SwhNEN